LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 27, 2021

ISUZU YADHAMINI MKUTANO MKUU WA ALAT +video

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT),Elirehema Kaaya akikabidhiwa zawadi na Afisa Masoko wa Kampuni ya uuzaji wa magari aina za Isuzu ya Al Mansour Auto. EA (Tanzania) Ltd, Ndeshi Rajab baada kutembelea banda la maonesho ya magari hayo kwenye viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo unafanyika Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi wa Viongozi wa kitaifa wa ALAT.

Isuzu inatambulisha magari yao aina ya DMAX na XRIDER ambayo ni Pick up double na single cabin. Manual na automatic zenye Diesel engine CC 2500 intercooler na turbo. Pia wanayo malori yenye tani 3.5 hadi 18.

Kampuni hiyo yenye ofisi zake Dar es Salaam, ni miongoni mwa wadhamini wa Mkutano Mkuu huo, ambao umefunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma leo.


Mkurugenzi wa Kampuni ya uuzaji wa magari aina ya Isuzu ya Al Mansour Auto. EA (Tanzania) Ltd, Anurup Chatterjee akizungumza na vyombo vya habari kuhusu udhamini wao wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT), na mpango wa kufanya nao biashara hiyo.

Katibu Mkuu wa ALAT, Kaaya akishuka kwenye gari  baada ya kukagua.

Mkurugenzi wa Isuzu, Chatterjee akiagana na Kaaya

Afisa Masoko wa Kampuni ya uuzaji wa magari aina za Isuzu ya Al Mansour Auto. EA (Tanzania) Ltd, Ndeshi Rajab akielezea zaidi kuhusu biashara hiyo ya magari.

Baadhi ya magari aina ya Isuzu 






 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini, Mkurugenzi  Chatterjee na Afisa Masoko wa kampuni hiyo ya uuzaji wa magari aina ya Isuzu, Ndeshi wakizungumzia biashara hiyo pamoja na udhamini wao....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri wa Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages