LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 5, 2021

KAMONGA, MFAUME WARIDHIKA NA MAENDELEO YA UJENZI BARABARA YA ZEGE LUDEWA

 MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ludewa, Bakari Mfaume wakikagua ujenzi wa kipande cha Barabara kuu ya kutoka Njombe kwenda wilayani humo na kujiridhisha na maendeleo yake.


Kamonga akipata maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara
ulipofikia baada Serikali kutoa sh. bil. 30 kukamilisha ujenzi.
Ujenzi wa Barabara hizo ukiendelea eneo la Lubonde













Na Richard Mwaikenda, Ludewa

MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga na Mwenzekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaza ya Ludewa, wamekagua ujenzi wa kipande cha Barabara kuu ya kutoka Njombe kwenda wilayani humo na kujiridhisha na maendeleo yake.


Akizungumza  alipofika katika eneo la ujenzi akitokea Bungeni Dodoma jana, Kamonga amesema kuwa licha ya ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa kwa zege kuchukua muda mrefu lakini sasa ujenzi wake unakwenda vizuri, unaridhisha.


"Mwenendo si mbaya kazi inaendelea vizuri, Km. 50 tayari ujenzi wake umekamilika bado Km 50 nyingine  tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu serikali kutoa sh. bil. 30 ya ujenzi Km nyingine 30, itakuwa bado sh. Bil. 20  ya kumalizia  Km 20 kukamilisha Km. 100," amesema Kamonga.



Kamonga amesema kuwa fedha hizo sh. Bil. 30 zimetolewa baada ya hivi karibuni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi, Godfrey Msongole  na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Dkt. Bernard Chamuriho kukagua ujenzi wa barabara hiyo unaofanywa na Kampuni ya Korea Kusini, Choan Kwong.



Ameyasema hayo walipokutana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa, Bakari Mfaume  na kwa pamoja kukagua berabara hiyo eneo la Lubonde ambapo waliwakuta wafanyakazi wa Kampuni hiyo, wakiendelea na kazi.


Akizungumza na viongozi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Mkazi wa Kampuni hiyo, Deng Ryeol na Mhandisi wa Vifaa vza Ujenzi, Heemin Park  waliwahakikishia kuwa pasingekuwa na mvua zinazo karibia kuanza hivi karibuni wangemaliza ujenzi Desemba mwaka huu, lakini sasa ujenzi wake utakamilika Julai mwakani.


Naye Katibu wa CCM Wilaza ya Ludewa, Mfaume ameishukuru Serikali ya Awamu ya 6 inazoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuwajengea barabara hiyo muhimu  ambayo hivi sasa ujenzi wake unaendelea vizuri na kwamba ikikamilika itawaletea unafuu wananchi wa wilaya hiyo.

 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages