Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga akizungumza alipokuwa akifungua Tamasha la mashindano ya ngoma ya asili ya Mganda wilayani Ludewa, Njombe.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lifua, akisisitiza amani na utulivu wakati wa mashindano ya ngoma ya Mganda yaliyofanyika kijijini hapo.
Mbunge Kamonga akiwa na baadhi ya viongozi wakiangalia mashindano hayo.
Mashindano ya vikundi mbalimbali vya ngoma ya Mganda yakiendelea kwenye uwanja wa Nkinila, Lifua.
Watoto wakijifunya kupiga ngoma kwa kutumia kandambili zao wakati wa mashindano hayo. PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, Ludewa
MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga ametoa ng'ombe kwa ajili kitoweo kwa wanaoshiriki Tamasha la mashindano ya ngoma ya asili ya Mganda jimboni humo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi Kamonga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo ya siku 3 ameipongeza kamati ya maandalizi kwa kufanikisha tamasha linaloshirikisha maboma 15 kutoka wilaya za Mbinga, Nyasa na Ludewa yenyewe.
Amesema kuwa mashindano hayo ya ngoma ya asili yaliyofanyika katika Kitongoji cha Nkinila, Kijiji cha Lifua Kata za ya Luilo ni muhimu sana kwani husaidia kujenga mahusiano, huleta burudani lakini pia amani na upendo na kwamba imo hata kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
"Kwa hiyo ndugu zangu Michezo , Sanaa na Utamaduni inasisitizwa sana kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Serikali yetu ina wizara mahususi ambayo husimamia mambo ya utamaduni, nimesikiliza nyimbo nimeona wanaimba nyimbo ya kudumisha amani upendo na mshikamano, ambao ulianzishwa wasisi wetu tokea miaka mingi, lakini michezo licha ya kuleta burudani, vile vile inatuburudisha na kujenga mauhusiano mema baina ya jamii,"amesema Kamonga.
Vikundi (maboma) vilivzoshiriki katika mashindano hayo ni:Wilaya za Ludewa;Lihagule,Luilo,Mseto,Idusi,Kiyoho, Nindi, Nsungu na Mzalendo. Nyasa ni;Lituhi,Taifa,Upendo, Uweyo na Shujaa na kutoka Mbinga ni Ndongosi na Lizombo.
Mdau ili nisikuondolee uhondo nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupotia clip hii za video Mwenzekiti wa Kijiji cha Lifua,Msafiri Haule, Diwani wa Kata za Luilo, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Kamonga na wananchi wakizungumzia tamasha hilo lakini na kuona pia tamasha hilo....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇