LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2021

UVCCM YAMPONGEZA RAIS KUENDELEZA UMOJA NA NCHI JIRANI

Katibu wa UVCCM, Kenen Kihongosi akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma, ambapo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kudumisha umoja na nchi jirani. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCC Mkoa wa Dodoma, Billy Chidabwa.
Katibu wa UVCCM, Kenen Kihongosi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma. Kushoto ni Maulid Bilal Katibu wa Oganaizesheni UVCCM Taifa na Billy Chidabwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma.
Kihongosi na Chidabwa wakitoka baada ya mkutano na waandishi wa habari.


Na Richard Mwaikenda, CCM Blog Dodoma


UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza umoja na nchi jirani kama ulivyokuwa kwa watangulizi wake.


Pongezi hizo zimetolewa Katibu wa UVCCM, Kenen Kihongosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma.


Aidha, Kihongosi amewapongeza vijana wa vyama vingine vya siasa vinavyounga juhudi za serikali za kukabiliana na juhudi za mapambano dhidi ya janga la Corona.


Ili kuendeleza umoja na ushirikiano huo,Kihongosi amesema kuwa UVCCM iko mbioni kuandaa mashindano ya michezo mbalimbali nchini, kwa vile michezo ni ajira na afya.


Amewaomba vijana wa vyama hivyo kwamba bila kujali itikadi zao wajitokeze kwa wingi mashindano hayo yatakapoanzishwa ili kubaini  nchini kubaini vipaji vyao.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages