|
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga Mwenge wa Uhuru tayari kuanza kukimbizwa katika mkoa huo baada ya kumaliza katika wilaya 7 za Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imefanyika leo asubuhi katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Nyerere, Kijiji cha Migori Iringa .
Akizunguma wakati wa kukabidhi, RC Mtaka amesema kuwa Mwenge huo maalumu wa Uhuru unaokimbizwa na vijana 6 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), umetembelea, umekagua, umezindua na kukabidhi miradi yenye thamani zaidi ya sh. bilioni 41 mkoani humo.
RC Mtaka amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani humo, viongozi walihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga na janga la Corona.
Aidha, RC Mtaka amesema kuwa wakati wa mbio hizo wananchi 666 walipima vvu ambapo waliogundulika kuwa na virusi ni saba, lakini pia uchangiaji damu ulifanyika.
Amewapongeza wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakiongozwa na Josephine Mwampashi kwa kazi kubwa waliyoifanya mkoani humo na kuahidi kasoro chache zilizojitokeza katika baadhi ya miradi watahakikisha wanazirekebisha.
Vilevile, amewashukuru wakimbiza Mwenge wa Mkoa huo pamoja na viongozi na wananchi kwa kushiriki vyema wakati wa mbio hizo za Mwenge zilizoambatana na kazi ya kutembelea, kuweka mawe ya msingi, kukagua, kufungua na kukabidhi miradi yenye thamani ya sh. mil. 41.
Alikabidhi vyeti kwa wakimbiza mwenge wa mkoa wakiwemo askari na maofisa mbalimbali waliofanikisha mbio hizo ikiwa ni kutambua mchango wao huo.
Akizungumza baada kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa Iringa, Queen Sendiga amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani humo utakagua, utaweka mawe ya msingi, kuzindua na kukabidhi miradi yenye thamani ya zaidi sh. bil. 14. |
|
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Josephine Mwampashi akiuaga Mkoa wa Dodoma tayari kwenda kuingia Mkoa wa Iringa. |
|
Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Dodoma, wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi Mwenge. |
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo tayari kuanza kukimbizwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akitoa taarifa ya mkoa huo mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.
Chipukizi wakitoa hamasa wakati wa mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.
Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga akiupokea Mwenge wa Uhuru ambao umeanza kukimbizwa Mkoani Iringa leo.
Viongozi wa Mkoa wa Iringa wakiupokea Mwenge wa Uhuru.
Baadhi ya wananchi walioshiriki wakati wa hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru ukianza kukimbiwa katika wilaya ya Iringa mkoani Iringa mara baada ya kukabidhiwa kutoka Mkoa wa Dodoma.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇