Baada ya kukata utepe, RC Mtaka amekuwa wa kwanza kuchanjwa, akifuatiwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Fatma Mganga, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Best Magoma, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, wabunge, viongozi wa dini, wanasiasa, wanahabari na wananchi kwa ujumla.
Pia katika tukio hilo aliletwa Mtanzania mwenye asili ya Kiasia, bibi mwenye umri zaidi miaka 90 aitwaye, Zelakano Ladek ambaye alikuja na ndugu zake wengi wenye asili hiyo.
Zoezi kama hilo lilikuwa linaendelea katika wilaya 7 za mkoa huo ambazo kila moja imepangiwa vituo vitatu vya kutolea huduma hiyo ambapo Dodoma Mjini ina vituo 7 na Mkoa mzima una vituo 28.
Mkoa wa Dodoma umeshapokea jumla ya dozi 50,000 za chanjo ya Corona.Utoaji chanjo utaendelea kwa kadri watu watakavyokuwa wanajitokeza.
RC Mtaka akionesha kadi ya kuthibitisha kwamba amechanjwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Best Magoma akimkabidhi kadi ya kuthibitisha kuchanjwa Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt Fatma Mganga.
Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akipata chanjo cha Corona.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Dodoma, akipata chanjo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Mehodist, Joseph Bundala akipata chanjo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Keisha akipata chanjo.
Bibi kizee wa asili ya kiasia, Zelakano Ladek akipata chanjo ya Corona.
Mwanahabari Mkongwe, Livingstone akipata chanjo.
Al- Karim Salim Mohamed akipata chanjo ya UVIKO 19 (Corona) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Al-Karim Saleh Mohamed akipatiwa chanjo cha Corona.Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakijisajili kwa ajili ya kupata chanjo ya Corona.
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakiwa wamejipanga tayari kuingia kuchanjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mmoja wa wazee akiondoka baada ya kupata chanjo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇