Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya CCM, Jijini Dodoma leo Agosti 3, 2021. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Dotto Kwilasa, DODOMA.
UMOJA wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), imewataka wananchi na hasa
Vijana kuyapuuza maandamano yaliyoandaliwa na Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (BAVICHA), ya kutaka kushinikiza Mahakama kumfutia mashitaka
Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.
Tamko
hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenani Kihongosi
alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya CCM, Jijini
Dodoma leo Agosti 3, 2021.
Amesema
kuwa kitendo hicho cha kuingilia uhuru wa Mahakama ni uvunjivu wa
sheria za nchi lakini pia ni hatari kwa usalama na amani ya nchi yetu ambayo
inatakiwa sote tuilinde.
Kenani
Kihongosi amewataka viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kuwafunza vijana wa Baraza la Vijana wa Chama hicho
(BAVICHA)wawe na adabu ya kuheshimu Sheria za nchi na kuacha kuvuruga
amani.
Hatua hii imekuja
kufuatia tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa BAVICHA John Pambalu
kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kukidhi matakwa yao huku likiwataka
Vijana wa Chama hicho kuandamana Agosti 5 kwa madai ya kudai demokrasia
kuhusu kesi inayokabili Mwenyekiti wao Freeman Mbowe.
Akizungumza
kwenye mkutano wake na Vyombo vya habari Jijini hapa,Katibu huyo wa
UVCCM-Taifa ameeleza kuwa ni aibu kwa watu wazima kuendelea
kung'ang'ania mambo ambayo hayawezekani huku akiwataka kufuata taratibu
za mahakama ikiwa wanahisi kuonewa.
Amesema
hakuna mtu aliye juu ya Sheria na kuwa na mamlaka ya kumtaka Mh. Rais
kufanya jambo au matakwa yao binafis kwenye nchi hii,kambali yeye n Nani
Wasitumie ajenda ya kisiasa kuhakibi Taifa letu
Licha
ya hayo amesema,"Wapinzani wanapaswa wajitafakari ,wabadilike na
kukubali kubadilisha aina ya Mfumo wa siasa wanaoutumia ,lazima katika
siasa kuna ushindani,wahakikishe wanakuwa Mabalozi wa amani nankuepuka
kuhamasisha vurugu,"amesema.
Kutokana
na hayo Kihongosi amewataka Wanachama hao wanaotaka kuandamana
kuendelea kufanya shughuli za Maendeleo kwa ajili ya manufaa kwa
familia zao badala ya kutumia muda huo kwa masuala yasiyo na msingi.
"Niwashauri tu vijana wenzangu, badala ya kuandamana muda huo tumieni kutafuta ugali wa familia zenu,"amesema.
Katibu
huyo ameeleza kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA lazima atambue kwamba nchi hii
inaongozwa na Sheria na kwamba siku zote wao wamekuwa wakijipambanua
kuwa wanataka Demokrasia Sasa anashangaa wanataka kuvunja Sheria na
kusahau kuwa kila mhimili unafanya kazi kwa namna yake.
"Mnapotaka
kuandamana kupinga kuhusu yanayomhusu Mbowe mmejiridhisha vipi kwamba
hana makosa,mna wajibu wa kutii sheria za nchi,"amesisitiza
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇