Na Lydia Lugakila, Misenyi.
Mbunge wa jimbo la Nkenge wilayani Misenyi Mkoani Kagera Florent Kyombo amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi alioufanya kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini, huku akitaja halmashauri ya Misenyi kunufaika na aliyekuwa mkurugenzi wa wilaya hiyo Innocent Mbandwa Mkandala aliyehamishiwa wilayani Biharamulo Mkoani humo kwa uongozi wake uliotukuka na kufanya halmashauri hiyo Kung'ara zaidi.
Mh, Florent Kyombo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kata za Kyaka Mushasha na Bulembo wilayani humo waliojitokeza kusafisha eneo la ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya hiyo.
"Tunashukuru Rais Samia Suruhu Hassan kwa kufanya mabdiliko ya wakurugenzi, na wengi wamebaki nje lakini mkurugenzi wetu amebaki ndani ya kazi Innocent Mkandala anahamishiwa wilaya ya Biharamulo ndani ya Mkoa huu tunasema asante mama yetu kwa imani na mkurugenzi hatuwezi badilisha ila tutamkumbuka kwa utendaji wake ulio mzuri" alisema mbunge Kyombo.
Mbunge huyo ameeleza kuwa mkurugenzi huyo atakumbukwa pia kwa usimamizi mzuri wa mapato na mtumizi katika wilaya hiyo,pamoja na usimamizi mzuri kwa wenzake waliomsaidia huku akimuomba mkurugenzi huyo kumfunda anayechukua mikoba yake ili waweze kufanya naye kazi vizuri, kama ambavyo yeye alikuwa na uchungu wa maendeleo kwa wilaya hiyo.
Mkurugenzi huyo amehamishiwa wilaya ya Biharamulo na mikoba yake kuchukuliwa na waziri Khachi Kombo.
Kwa upande wao baadhi watumishi wa halmashauri hiyo akiwemo Julian Joseph Tarimo mkuu wa idara ya mipango takwimu na ufuatiliaji, amesema tangu ahamie katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mwaka 2020 mwezi Desemba amebahatika kufanya kazi na Mkurugenzi Mtendaji huyo kwa kipindi cha miezi 7 na kujionea utendaji wake ulivyo wa tofauti.
"Mukandala ni tofauti kabisa na wakurugenzi wote niliowahi kufanya nao kazi kwanza ni mkurugenzi mchapa kazi mwadilifu mwenye hofu ya Mungu na anayejali maslahi ya wananchi haki za watumiaji pia ni mtu aliyependa kufahamu idara zake zinavyofanya kazi na mfuatiliaji wa miradi ya maendeleo na asiyetaka ubabaishaji zaidi ni mtu aliyekuwa kunyoosha mambo na asiyependa ubabaishaji, binafsi namtakia kila la kheri kwenye kituo chake kipya akaendeleze yale mazuri aliyoyafanya wilayani Missenyi" alisema Tarimo.
Hata hivyo kwa upande wake mkurugenzi huyo Innocent Mkandala amewashukuru watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kipindi chote.
Ikumbukwe kuwa Agosti 2, 2021 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakurugenzi watendaji wa halmashauri za jiji, Manispaa, na wilaya
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Innocent Mkandala akiwashukuru Watendji wa Halmashauri hiyo pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliuounyesha kwake.kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇