LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 16, 2021

RAIS SAMIA KWENDA NCHINI MALAWI LEO KUSHIRIKI MKUTANO WA 41 WA WAKUU WA NCHI ZA SADC

Rais samia Suluhu Hassan

Ikulu, leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu Agosti 15, 2021 anatarajia kuondoka Jijini Dodoma kwenda nchini Malawi kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17 – 18 Agosti, 2021.


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jaffar Haniu, imesema katika taarifa aliyotuma kwenye vyombo vya habari leo, kuwa Mkutano huo wa 41 pamoja na mambo mengine, Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, watathibitisha nchi ya Malawi kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja (Agosti 2021 – Agosti 2022).


Haniu amesema matangazo ya kuwasili Rais Samia nchini Malawi na Mkutano huo yatatangazwa moja kwa moja, kupitia televisheni mbalimbali za hapa nchini na katika mtandao wa Youtube Channel ya Ikulu Mawasiliano.


Blog ya Taifa ya CCM (Official CCM Blog) tunamkia Rais Samia Safari njema na Mkutano mwema.

1 comment:

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages