LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 16, 2021

RAIS SAMIA AONDOKA LEO JIJINI DODOMA KWENDA NCHINI MALAWI KWENYE MKUTANO WA SADC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Samia Suluhu Hassan akipokea saluti ya Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo, wakati akiana naye kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma akiwa tayari kuondoka Nchini kwenda Nchini Malawi kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), leo. Mkutano huo utafanyika kuanzia kesho hadi keshokutwa (17-18 Agosti, 2021).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkamu wa Rais Dk. Philip Mgango, katika Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, muda mfupi kabla ya kuondoka Nchini kwenda Nchini Malawi kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), leo. Mkutano huo utafanyika kuanzia kesho hadi keshokutwa (17-18 Agosti, 2021). Wapili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipunga mkono kuwaaga viongozi waliomsindikiza kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, baada ya kupanda Ndege, tayari safari ya kwenda Nchini Malawi kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), leo. Mkutano huo utafanyika kuanzia kesho hadi keshokutwa (17-18 Agosti, 2021). (Picha ya Ofisi ya Makamu wa Rais).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages