LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 16, 2021

HICHILEMA WA CHAMA CHA UPND ASHINDA KITI CHA URAIS NCHINI ZAMBIA

Hakainde Hichilema


Lusaka, Zambia
Kiongozi wa  chama cha upinzania cha Chama Cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema ameshinda kiti cha Urais kwenye Uchaguzi Mkuu nchi humo.

Hichilema ameibuka mshindi baada ya kujizolea kura 2,810,777 akimbwaga mpinzani wake kutoka chama tawala Edgar Lungu aliyepata kura 1,814,201.

Hivi karibu kabla ya Tume ya Uchaguzi nchini Zambia Edger Lungu alidai kwmaba Uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Lungu alisema kwamba maafisa wa Chama chake Cha Patriotic Front walifukuzwa kutoka katika vituo vya kupigia kura, wakiacha vituo hivyo pasipokuwa na ulinzi wa kura.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages