LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 2, 2021

DODOMA YAPOKEA CHANJO 50,000 YA CORONA, UZINDUZI KUFANYIKA KESHO

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dodoma leo, kuhusu uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19 uatakaofanyika kesho Agosti 3,2021 katika Hospitari ya Rufaa ya Mkoa huo.  Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Fatma Mganga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Best Magoma akielezea utaratibu wa uzinduzi wa chanjo hiyo na watu watakaopewa kipaumbele.

Mtandao unaotumika kujisajili kupata chanjo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akizungumza katika mkutano huo kuwa CCM mkoa huo wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanjwa.



Baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa wakiwa katika kikao hicho.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo wakiwa katika kikao cha maandalizi ya uzinduzi wa chanjo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma

Uzinduzi wa watu kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa Mkoa wa Dodoma unaanza kesho Agosti 3 katika vituo 28 vilivyoandaliwa katika wilaya 7 za Mkoa huo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema Mkoa huo tayari umepokea chanjo 50,000 aina ya Janssen.


Amesema wataokapewa kipaumbele ni wahudumu wa afya,  watu wenye umri zaidi ya 50 na watu wenye magonjwa sugu kama moyo, kisukari na pumu.


RC Mtaka, amesema kuwa licha ya waliojisajili kupitia mtandao  kuchanjwa, lakini hata wasiojisajili wataandaliwa utaratibu maalumu mradi wanatimiza vigezo.


"Msiogope kwenda kupata chanjo, mimi nilishachanjwa Nairobi Kenya Mwaka jana, kwa umuhimu wa chanjo hiyo, mamangu nimemtoa Mara hadi hapa atakuwa miongoni mwa watakaochanjwa kesho," amesisitiza RC Mtaka.


Ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanjwa katika vituo Maalumu vilivyopangwa. Uzinduzi rasmi utafanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuanzia saa 3 asubuhi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa CCM mkoa huo wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya UVIKO 19 na kutoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutoogopa bali wajitokeze kwa wingi kwenda kupata chanjo .


Naye Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilaya ya Dodoma Mjini, George Saria amesema kuwa katika janga la mapambano dhidi ya Corona watu wote waungane bila kujadli itikadi za vyama wala dini wajitokeze kwenda kupata chanjo kwa usalama wa watanzania wote.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt, Best Magoma amekiri kuwepo kwa wagonjwa wa Uviko 19 katika mkoa huo na kueleza kuwa chanjo hiyo iko salama na yeye atakuwa wa kwanza kwenda kuchanjwa.



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages