Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akiwasilisha Taarifa ya Mkoa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanzia Januari hadi Juni 2021 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo leo Agosti 25,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa akielezea kuhusu ziara ya Kamati ya siasa ya mkoa huo iliyofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho katika wilaya zote za mkoa huo.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deo Ndejembi.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akiutaka uongozi wa mkoa kushirikiana kuwaondoa kwenye minada mawakala wa mazao wanaowadhurumu wakulima na wafugaji.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma, Mary Ngozi akitoa nasaha zake wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Dodoma, Neema Majule akiwa mmoja wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma waliohudhuria kikao hicho.
Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Mkanwa akitangaza maazimio ya kikao hicho.
Spika Ndugai akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mwenendo wa kikao hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dodoma kutoka Kongwa, ambaye pia ni mkulima, Anderson Sangara akiuomba uongozi wa mkoa kuanzisha duka la kuuza pembejeo na mbegu za mazao za uhakika kutoka kwa wakala wa mbegu ASA ili kuepukana na kuuziwa mbegu feki. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Shukrani hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa alipokuwa akihitimisha kikao cha uwasilishwaji wa Taarifa ya mkoa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia Januari hadi Juni 2021 uliofanywa na Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka Agosti 25, 2021.
Aidha, Mkanwa akitoa maazimio ya kikao hicho, ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kutoa sh. Bil. 131, za kugharamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika jiji la Dodoma ambalo ni makao makuu ya nchi.
"Bil. 131 za ujenzi wa miundombinu katika jiji la Dodoma ni fedha nyingi, zitengewe vema na zitumike kama ilivyokusudiwa," amesema Mkanwa na kuongeza kuwa Mkoa wa Dodoma upo bega kwa bega na Rais Samia kumsaidia katika harakati za kuliletea Taifa maendeleo na kumuombea afya njema katika utumishi wake.
Amesema kuwa maazimio mengine ni; kuhakikisha miradi yote yenye changamoto, Halmashauri inatoa maelekezo ikamilike haraka na iwe na ubora unaostahili, vile vile maagizo yote waliyoyatoa kwenye kamati ya pamoja ya mkoa yatekelezwe.
Wameshauri kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu tahadhari dhidi ya janga la Corona na kuhamasisha wananchi kukata shauri kwenda kupata chanjo.
Wametoa pongezi kwa viongozi wa wilaya na mkoa kwa ushirikiano mkubwa walioutoa wakati kamati ya siasa ya mkoa huo ilipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho mkoani humo ikiwa ni kuitikia agizo la Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aliyetoa siku 14 kwa kamati zote za siasa za mikoa kufanya ziara hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ambaye amepongezwa kwa uongozi wake mzuri na ulio shirikishi, ameahidi changamoto zilizopo kuzifanyia kazi ikwemo maagizo na ushauri waliopewa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇