LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 25, 2021

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE KWA MSIBA WA ASKARI WANNE WALIOUAWA DAR

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pole kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, Inspekta Generali wa Polisi, familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya askari watatu wa Jeshi la Polisi na askari mmoja wa kampuni ya ulinzi ya SGA vilivyotokea leo tarehe 25 Agosti, Jijini Dar es Salaam.

 

Mhe. Rais Samia amewataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati huu ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo la kihalifu lililotokea katika makutano ya Barabara ya Kenyatta na Kinondoni.

 

Aidha, Mhe. Rais Samia amewaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao.

 

Pia Mhe. Rais amemuomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za Marehemu Mahali pema Peponi, Amina.

 

 


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages