Taarifa ya vifo hivyo imetolewa leo Agosti 25, 2021, na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas, alipofika eneo la tukio.
Aidha, kufuatia tukio hilo Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa familia za Askari wanne akiwemo yule wa kampuni ya ulinzi ya SGA waliofariki baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwashambulia katika eneo la Selander, karibu na Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, ameagiza polisi kuchunguza kwa kina na kusema mtu huyo amedhibitiwa na hali ni shwari.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇