BENKI
ya NMB imeshinda tuzo mbili za Kimataifa za umahiri kwa kutambulika
kuwa benki bora nchini, ushindi uliotolewa na majarida makubwa duniani
yanayoaminika katika kufanya tafiti za kifedha na mabenki.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema, tuzo ya kwanza iliyotolewa kwa benki
hiyo ni tuzo ya EuroMoney ambayo ni mara ya tisa kwa benki hiyo kushinda
tuzo hiyo kutokana na ufanisi, utendaji na ubunifu wa benki hiyo.
Amesema,
tuzo ya pili iliyotolewa na jarida la Global Banking and Finance
imeitambua benki ya NMB kwa huduma bora kwa wateja binafsi na biashara
za kati kwa mwaka 2021.
Zaipuna
amesema kuwa hiyo ni heshima kubwa na kielelezo cha ufanisi wa benki
hiyo na wameheshimu na kuthamini heshima hiyo na tuzo hizo zinatokana na
juhudi zinazofanywa na benki hiyo na kutambuliwa ndani na nje ya nchi.
Kuhusiana
na vigezo vilivyotumika na benki hiyo kuibuka kinara, Zaipuna amesema
vigezo hivyo ni pamoja na ufanisi na utendaji, usalama wa huduma za
kimtandao, mtaji na uwajibikaji wa benki hiyo kwa jamii.
Pia
amesema benki hiyo itaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi wa
hali ya juu katika kuhakikisha wanatoa huduma bora na viwango vya juu
kwa jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇