LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 2, 2021

ALIYEKUWA MBUNGE MTEULE KWA TIKETI YA CCM JIMBO LA KONDE PEMBA SHEKHA MPEMBA FAKI AJIUZULU, CCM YATOA TAMKO

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla alipokuwa akimnadi Sheha Mpemba Faki wakati wa ufungaji wa kampeni za CCM za Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo, Julai 17, 2021. (Picha na Maktaba ya CCM Blog)


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya aliyekuwa Mbunge wake mteule wa Jimbo la Konde Pemba, Visiwani Zanzibar Shekha Mpemba Fakhi kujiuzulu baada ya kuchaguguliwa katika Uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 18 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekua Mbunge wa jimbo hilo Khatibu Haji.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, imesema CCM imepokea barua ya Mbunge huyo kujiuzulu, Mbunge huyo akieleza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo Shaka amesema Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kuwa ni haki yake ya Msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM. Ifuatayo ni taarifa ya CCM kuhusu Mbunge huyo kujiuzulu.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages