LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 23, 2021

ASKOFU GWAJIMA ATINGA BUNGENI KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI




Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma

ASKOFU Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,  akiwasili bungeni Dodoma huku akisindikizwa na askari, tayari kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.


Amewasili  mchana huu majira ya Saa 6:36 kupitia lango Kuu la kuingilia wabunge  na kupokelewa na askari hao walimuongoza hadi eneo la mapokezi jengo la Utawala.

 

Askofu Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, ameitwa mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.


Mbunge mwingine aliyeitwa kwa tuhuma kama hizo ni Jerry Silaa wa Jimbo la Ukonga ambaye atahojiwa na Kamati hiyo kesho Agosti 24, 2021.

Askofu Gwajima akiwa katika mitambo ya ukaguzi jengo la Utawala la Bunge.
Wanahabari wakiwa kazini
Askofu Gwajima eneo la mapokezi Jengo la Utawala akisubiri kuitwa kwenye kikao.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages