LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 23, 2021

WATANO TRA WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI WAKIFUKUZA GARI WALILOSHUKU LINAMAGENDO, LEO

 CCM Blog, leo

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamefariki dunia kwa ajali ya gari leo saa 11 alfajiri katika eneo la Hanseketwa Old Vwawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe.


Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo mkoa huo Janeth Magomi amesema, ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Toyota Land Cruiser kugongwa kwa nyuma na lori la mizigo aina ya Fuso.


Taarifa zimesema Wafanyakazi hao ni kikosi kazi cha 'Fast Track' cha TRA na walikuwa wanafukuzana na gari walilokua wanalishuku kuwa limebeba bidhaa za magendo ambalo halikulitaja.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages