Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akizungumza na Viongizi wa UWT na CCM katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM, Wilaya ya Ilala, jana ikiwa ni mwendekezo wa ziara alizozianza hivi karibuni kutembelea wilaya zote za mkoa huo. (Picha na Bashir Nkoromo).
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Ziara za Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga katika wilaya za mkoa huo, imeendelea kuzaa matunda baada jana kuingiza jumla ya Sh. Milioni 6,200,000 zilizochangwa katika mkutano wake Wilayani Ilala, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT katika mkoa huo.
Katika ziara hizo ambazo Mwenyekiti huyo anaambana na Kamati ya Utekekezaji ya UWT mkoa, zinalenga kuwashukuru Wanachama wa UWT kwa kumchagua, kuimarisha Uhai wa Jumuiya na Chama na kufanya harambee katika mikutano wakati wa ziara hizo kwa ajili ya kupata fedha na vifaa kwa ajili ya kutimiza azma ya kujenga nyumba 5 katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam na moja ngazi ya mkoa za Watumishi wa UWT.
Akiyangaza kilichopatikana baada ya harambee, katika mkutano wa ziara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala na kuhudhuriwa na Viongozi wa ngazi mbalimbali wa UWT na wa CCM), Katibu wa UWT mkoa Grace Haule alisema kiasi hicho kilichopatikana cha Sh. Milioni 6.6, sh. 600,000 ni fedha taslimu na ahadi sh. milioni 5.6.
Grace alisema mbali na michango ya fedha pia katika harambee hiyo zilipatikana ahadi za michango ya matofali 2,900 na nondo tani moja.
Baada ya kutangaza kilichopo Grace alifafanua namna ya viongozi kuhifadhi fedha za Jumuiya hiyo ili ziweze kuwa salama na kutumika vema kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa UWT mkoa Florence Masunga Jumuita hiyo mkoa wa Dar es Salaam, imepanga kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa ajili ya Watumishi wake Novemba mwaka huu kwa gharama ya Sh. Bilioni 1.3, kwa nyumba zote.
"Tumeamua tuanze kuchangishana wenyewe kwenye mikutano ya ziara zetu, baadaye ndiyo tutashirikisha wadau wengine kutuchangia pale tutakapokuwa tumeoelewa", amesema Florence Haule
Akizungumza na Wanachama, Watendaji na Viongozi wa UWT na CCM kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, aliuelezea kwa kina mpango wa ujenzi wa nyumba hizo, akisema zitakuwa zenye hadhi ya kisasa na stahili bora kwa kuishi mtumishi wa Jumuiya hiyo.
Florence aliwataka Wanachama wa Jumuiya hiyo, kupambana katika uchangiaji fedha za ujenzi wa nyumba hizo ili kuudhihirishia umma kwamba Wanawake wanaweza na wakiwa na jambo lao haikwami.
Alisema, pamoja na lengo kuu la ziara zake katika wilaya zote kuwa ni kuhamasisha uchagiaji wa ujenzi wa nyumba hizo, lakini pia ni kuwahamasisha Wanawake kuzitumia fursa za mikopo zilizopo ili kuinua vipato vyao, familia zao na taifa kwa jumla.
Habaripicha👇
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi akizungumza wakati waMkutano huo.
Mwendeshaji wa Mkutano huo, akiongoza maombi ya Kiislam mwanzoni mwa mkutano huo.
Mmoja wa Wajumbe wa Mkutano huo akiongoza Maombi ya Kikristo mwanzoni mwa Mkutano huo
Katibu wa Kamati ya Uchumi na Fedha UWT mkoa wa Dar es Salaam, Abriat Kivea ajitambulisha wakati wa Mkutano huo. Katikati ni Katibu Msaidizi Grace Mukumbwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Herriet Mwakifulefule.
Mmm
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakati akizumgumza kwenye Mkutano huo.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam wakati akizumgumza kwenye Mkutano huo.
Wajumbe kutokaUWT mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wakati akizumgumza kwenye Mkutano huo.Keki ya zawadi ikipelekwa kwa Mgeni rasmi Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florenge Masunga wakati wa mkutano huo.Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar Salaam Florence Masunga akipokea zawadi hiyo ya Keki maalum kutoka UWT Wilaya ya Ilala.Kina Mama wa UWT Wilaya ya Ilala wakimpongeza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga wakati wa mkutano huo.Diwani Viti Maalum (UWT) Saada Mandwanga akitangaza mchango wake kuchangia ujenzi wa nyumba za Watumishi wa UWT katika Wilaya zote mkoani Dar es Salaam na moja ngazi ya mkoa, wakati wa mkutano huo. Mama Mandwanga aliahidi kutoa tani moja ya saruji na nondo kadhaa.
Wajumbe wengine wakiselebuja kushangilia uchangiaji huo wakati Wajumbe mbalimbali waliookuwa wakiendelea kutoa michango ya pesa taslim na ahadi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo za Watumishi wa UWTMjumbe mwingine Dk. Shaimaa Mohammed Nawwar (Kushoto) akiwa ameitwa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kutangaza mchango wake wa ujenzi wa nyumba hizo na kueleza pia kwamba Hospitali anakofanya kazi Kisutu Polyclinic inatoa kifurushi maalum cha Bima ya Afya kwa kinamama.Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule na Mjumbe wa Baraza la UWT mkoa huo Marium Machicha, wakijumlisha jumlisha michangoa ya fedha taslim na ahadi baada ya hatabee kumalizika wakati wa Mkutano huo.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWT. Mkoa huo Florence Masunga wakati wa mkutano huKatibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akutanza kilichopatikana katika haramvee ya kuchagia ujenzi wa nyumba za watumishi wa UWT wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence akitoa neno la shukrani wa kwa wote waliofanikisha mjutano huo kwenda vizuri ikiwa ni pamoja na wengi kujitoa kutoa michango yao kuchangia ujenzi wa nyumba za watumishi wa UWT.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇