LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 24, 2021

WAZIRI MKENDA AZINDUA KAMPUNI YA PASS LEASING YA KUKOPESHA ZANA ZA KILIMO BILA DHAMANA

Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kampuni ya Pass Leasing itakayokuwa inajishughulisha na kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji zana za kilimo bila dhamana kwa riba nafuu katika hafla iliyofanyika wakati wa Wiki ya Pass Trust kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma Julai 24,2021. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Athony Mtaka na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida.

Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda  (kulia), akimkabidhi ufunguo Anthony Maganga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 ikiwa ni mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka (kulia), akimkabidhi  namba yAnthony Maganga ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland yenye thamani ya sh. nil. 54 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda, akimkabidhi ufunguo Lillian Maricky wa Kampuni ya Magic LN Suppliers ya Chalinze, mkoani Pwani ikiwa ni ishara ya kumkabidhi mitambo ya kuvuna mpunga  yenye thamani ya sh. mil.79 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda  (kulia), akimkabidhi ufunguo  Gebe Millinga  ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya John Deere pamoja na majembe yake lenye thamani ya sh. mil. 71.4  mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Pass Trust, Dkt. Tausi Kida. Gebe amepokea trewkta hilo kwa niaba ya kaka yake  Mwanzo Millinga anayefanya kazi ya kilimo  mkoani Ruvuma.
Waziri wa Kilimo. Profesa Adolph Mkenda   akimkabidhi ufunguo Dickson Tesha  ikiwa ni ishara ya kumkabidhi trekta aina ya New Holland lenye  thamani ya sh. mil. 46 mkopo uliotolewa na Kampuni ya Pass Leasing. Tesha amepokea trekta hilo kwa niaba ya Japhet Ndebesi wa Chamwino, mkoani Dodoma.





Na Richard Mwaikenda, Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolph Mkenda amezindua Kampuni ya Pass Leasing ya kukopesha wakulima zana za Kilimo bila dhamana na kwa riba nafuu.

Baada ya kuzindua amekabidhi zana za kilimo za kisisa kwa wateja wanne wa kwanza ambazo ni matrekta matatu na mtambo wa kuvunia mpunga.

Waliokabidhiwa ni; Kampuni ya Magic LN Suppliers ya Chalinze mkoani Pwani ambayo imekopeshwa mtambo wa kuvunia mpunga wenye thamani ya sh. Mil. 79, Anthony Maganga wa Igunga Tabora aliyepata Trekta aina ya New Holland lenye thamani ya sh. Mil. 54.

Wengine ni Japhet Ndebezi wa Chamwino mkoani Dodoma aliyekopeshwa Trekta lenye thamani ya sh. Mil. 46 na Mwandishi wa Habari Mwanzo Millinga wa Ruvuma ambaye amepata Trekta aina ya John Deere pamoja na majembe yake lenye thamani ya sh. Mil. 71.4.

Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka na viongozi wa Taasisi Pass Trust pamoja na wananchi waliohudhuria Wiki ya Pass Trust kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Mikopo inayotolewa na Kampuni ya Pass Leasing kwa upande wa kilimo ni; zana za kuwezesha uzalishaji wa kilimo cha mazao, usindikaji, uhifadhi wa mazao na usafirishaji.

 Kwa upande wa uvuvi ni; vifaa uvuvi na mashine zote zitumikazo kuongeza tija katika sekta ya uvuvi. Ufugaji nyuki ni; Vifaa mbalimbali  vya kuongeza tija na thamani katika sekta ya nyuki na  mazao yatokayo na  na nyuki.

Ufugaji ni; Vifaa na mashine za kuongeza tija katika sekta ya ufugaji na kwa upande wa misitu ni vifaa na mashine zitumikazo kwenye misitu na viwanda vya mbao.



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages