LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 4, 2021

SEKRETARIETI YA CCM IKIONGOZWA NA KATIBU MKUU CHONGOLO YAWASILI ZANZIBAR, YAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA DK. SHEIN, LEO.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (Watatu kushoto) na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, nyumbani kwake mjini Zanzibar, leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akijitambulisha rasmi na kuwatambulisha Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongoli akiendelea na utambulisho.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, nyumbani kwake mjini Zanzibar, leo. 
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wakiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzani (UWT) Queen Mlozi wakiwa katika mazungumzo hayo nyumbani kwa Dk. Shein.

Dk. Shein akizungumza machache na Shaka Hamdu Shaka kabla ya msafara wa Chongolo kuondoka nyumbani kwake.

Chongolo alipowasili Zanzibar👇
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo Naibu Katibu wa CCM Bara Christina Mndeme na Katibu wa NEC Oganaizesheni Moudline Castico (kulia) walikishuka kwenye Boti walipowasili katika Bandari ya Malindi jijini Zanzibar, mapema, leo.

NmKatibu Mkuu wa CCM akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Mabodi ambaye aliupokea msafara ulipowasili katika Bandari ya Malindi,. Zanzibar, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akisalimiana na viongozi waliompokea na msafara wake katika Bandari ya Malindi, Zanzibar alipowasili. Kulia kwa Chongolo ni Baibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdallah Juma Mabodi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme.

 ©CCM Blog/2021

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages