MAOMBI YA KUJIUNGA NA CHUO SEPTEMBER, 2021/2022
____________
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika kampasi zake za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa muhula wa Septemba 2021/2022
Chuo kinatoa STASHAHADA (DIPLOMA) katika fani za Uhasibu (Accountancy), Masoko (Marketing Management) Usimamizi wa Biashara (Business Administration), Manunuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management), Vipimo na Mizani (Metrology and Standardization) na TEHAMA (Information and Communication Technology) na Shahada ya Ualimu na Biashara
1.stashahada (Diploma) miaka 3
Awe amehitimu kidato cha nne na mwenye ufaulu wa angalau alama“D” nne, au mwenye NVA level 3.
2.Stashahada (Diploma) miaka 2
Awe amehitimu kidato cha sita na mwenye ufaulu wa angalau alama “E” (Principal pasimoja) na“S” (Subsidiary pasi moja), Au amefuzu ngazi ya cheti katika chuo kinachotambulika na Serikali.
3.Shahada (Bachelor Degree)
Awe amehitimu kidato cha sita na mwenye ufaulu wa angalau principle pass 2 zenye jumla ya alama 4 na kuendelea kutoka katika masomo mawili unganishwa Au amefuzu ngazi ya cheti katika chuo kinachotambulika na Serikali/NACTE na awe na GPA ya kuanzia 3.0
Dirisha la maombi kwa njia ya mtandao liko wazi .
Tembelea Tovuti ya Chuo www.cbe.ac.tz Au fika katika kampasi zetu kama ifuatavyo/au piga simu hizi
-MWANZA Eneo la Ilemela ( Mecco Kangaye)
0759 924 626 /0659 707 000
-DAR ES SALAAM (Mtaa wa BIBI Titi Mohammed)
0756 722 467 /065 525 0115
-DODOMA (Eneo la Mtaa wa makole Karibu na jengo la Bunge
0754 940 660/ 0767 097 463
-MBEYA Eneo la Uzunguni “B” Mkabala na Hoteli ya Rift Valley
0756 516 771 / 0716 803 664 / 0768610505
Mikopo ya Elimu inapatikana kwa programme zote (Mwanza)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇