Tegeta, Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wa Makanisa, wamekuwa wakijitokeza haradhani au kwa njia zingine kuwakosoa viongozi mbalimbali wanapokuwa wanadhani viongozi hao wa nchi wamekosea.
Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta, Dar es Salaam, lenyewe limeonesha kuwa na mtazamo tofauti, likisema kwamba Kazi ya Viongozi wa Dini hususan Kanisa ni kinyume kwao kuchukua kszi ya kuwakosoa viongozi.
Kanisa hilo, likinukuu vifungu vya Maandiko katika Biblia, limesema , "Kazi ya Kanisa siyo kukosoa kiongozi, MUNGU BABA aliyemuweka atamwelekeza Yeye. Ushuhuda katika hili ni Mfalme Sulemani aliyeongoza Taifa la Israeli kwa hekima aliyopewa na MUNGU BABA (1Wafalme 3:9-13).,
Ili kuijua kwa undani, hoja hiyo ya Kanisa Halisi la Mungu Baba, endeleo kusoma kama alivyoandika Baba Wa Uzao wa Kanisa hilo. 👇
WAJIBU WA KANISA KWA JAMII NA TAIFA
Lango la 26 Adari, Vol.2 (23 Mei, 2021), tulifanya ibada Jijini Mbeya kuweka wazi kuwa tatizo linapotokea katika Taifa au Mkoa na Wilaya, viongozi wa Mkoa na Wilaya hawana shida; ni falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho chafu na anayetakiwa kuliondoa ni Kanisa (Efeso 3:10).
Kanisa tumepewa mamlaka na CHANZO HALISI CHA MEMA kufuta falme na mamlaka ambazo ndizo zinaleta matatizo katika jamii. Hivyo, Kanisa ndilo linatakiwa kuondoa hizo falme na mamlaka katika eneo husika. Ndiyo maana katika ibada hiyo tulikubaliana tusiwakosoe viongozi wala tusiwanung’unikie au kuwalaumu kwa sababu matatizo yanapotokea sio wao, ni falme na mamlaka za giza (Efeso 6:12).
Wajibu wa Kanisa kwa anayebeba Moyo wa Taifa na wasaidizi wake ni kuwaombea dua, sala, shukrani kwa mujibu wa Sauti ya MUNGU BABA-CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI.
Katika 1Timotheo 2:1-3 imeandikwa kuwa;’’ kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utawala wote na ustahivu hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za MUNGU BABA mwokozi wetu’’.
Tunawaombea viongozi ili haya matatu yatokee kwa uhalisia katika Kanisa, jamii na Taifa:
Utawala wa Amani (Isaya 2:4,1Falme 5:4);
Upendo usiobagua (Efeso 4:5-6; 1Korintho 13:13c); na Ibada ni uzalishaji (Mwanzo 2:15).
Jambo kubwa tunalotakiwa kufanya kwa Kiongozi wa Nchi, Mawaziri, Wabunge, Majeshi ya Ulinzi wa Taifa na Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Maafisa Tarafa na Kata; Viongozi wote wa Mitaa, Vijiji, Vitongoji huwa ni kuwainua wawe na afya njema; hekima katika uongozi zaidi ya Mfalme Sulemani katika 1Falme 3:9-13. Aidha, tunatakiwa kuwainua wafanikiwe katika miradi ya maendeloeo ya taifa wanayofanya kwa ajili ya wananchi.
Kanisa tunatakiwa kutambua kuwa kiongozi aliyeko madarakani amewekwa na MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI aliyeumba kila kitu juu ya nchi. Katika Rumi 13:1-4, inathibitisha kuwa Viongozi wamewekwa na MUUMBA WA VYOTE, WOTE NA YOTE ili watuletee mema na mazuri. Hivyo, wajibu wa Kanisa ni kumwinua kiongozi ili Aliyemuweka katika hiyo nafasi, kwa ajili ya mema na mazuri aliyoyapanga ndani ya TAIFA, yatimie.
Kazi ya Kanisa siyo kukosoa viongozi, MUNGU BABA aliyemuweka atamwelekeza Yeye. Ushuhuda katika hili ni Mfalme Sulemani aliyeongoza Taifa la Israeli kwa hekima aliyopewa na MUNGU BABA (1Wafalme 3:9-13).
Kwa mujibu wa Hesabu 12:1-13, Kanisa litambue kuwa ni kosa, kumkosoa Kiongozi au kumsema vibaya. Inakuletea magonjwa yasiyopona, kazi zako kuharibika, maisha yako kutokuwa na mwendelezo mzuri. Maana Wana wa Israeli walipotoka Misri walikuwa wakiongozwa na Musa akiwa kiongozi wao mkuu, walipomkosoa tu kwa kuoa Mwafrika walipigwa na ukoma saa hiyo hiyo.
Haruni naye kwa kitendo cha kumkosoa Musa, ukuhani wake uliishia pale akaambiwa vazi la ukuhani ampe mwanaye Eliazeri. Kanisa kwa kutambua hili, hatutakiwi kumkosoa kiongozi, bali tunatakiwa kumwinua kama tulivyosoma katika 1Timotheo2:1-4. Kama wewe ni Mfanya biashara ukikosoa viongozi biashara inakufa; Mkulima ukimkosoa kiongozi hutapata mavuno shambani; Mwanafunzi ukimkosoa kiongozi unafeli katika masomo yako:
Hatutaki tuwe na magonjwa mabaya ya ukoma kama Miriamu wala hatutaki kazi zetu ziharibike. Hivyo, sote tuwe na msimamo kuwa kiongozi hakosei wala hakosolewi maana ukimkosoa unakuwa umemkosoa MUNGU BABA kwa mujibu wa Rumi 13:1-3. Unatakiwa kumuinua apate kutenda mema, maana MUNGU BABA ameweka kiongozi kwa ajili ya kutuletea mema. Hivyo, kumkosoa aliyewekwa mbele yako kukuletea mema, utakuwa umekataa hayo mema aliyopewa kwa ajili yako.
Wakati wa Mfalme Daudi yupo mmoja aliyejaribu kumkosoa Mfalme Sauli aliyemtangulia Daudi, Daudi alimpa adhabu ya kunyongwa (2 Samweli 1:14-16). Ili usiwe na mauti katika kazi zako, usimkosoe kiongozi. Hata kama kiongozi hatakuchukulia hatua, yule aliyemuweka kwenye uongozi ambaye ni MUNGU BABA hatakuacha. Katika Isaya 37:36, kuna waliojaribu kumkosoa Mfalme Hezekia, MUNGU BABA akatuma Malaika akawaadhibu ingawa Mfalme Hezekia hakuwachukulia hatua yoyote kama yeye.
Katika Yeremia1:12, kitabu kinasema kuwa MUNGU BABA anaangalia sauti yake apate kuitimiza. Hivyo, kila Kuhani na Uzao ajue wajibu wake kwa viongozi siyo kuwakosoa bali kuwaombea dua, sala, maombezi na shukrani wawe na afya nzuri, wapewe nguvu na hekima kuongoza Taifa, waepushwe na wabaya wote, wapate wepesi katika kazi.
Kwa mujibu wa Rumi 15:30-31, tunapaswa kuwaombea viongozi wote wapate kibali, wapendwe na wale wanaowaongoza, hiyo ndiyo kazi ya Kanisa. Kama hukuomba wala hukushukuru kwa ajili ya kiongozi, usilaumu wala kukosoa. ubarikiwe kwa kupokea.
Sawa kabisa
ReplyDeleteMUNGU BABA ATUPE MOYO WA SHUKRANI KATIKA MAMBO MEMA YOTE ZABR 100:4
ReplyDeleteKweliiii halisi
ReplyDeleteImekuwa. Uaminifu wetu katika madogo tuliyopewa kwa kushukuru. Utasababisha MUNGU BABA CHANZO HALISI Cha MEMA YOTE atupe makubwa zaisi. Tusiposhukuru tutavikwa kongwa la maangamizo. Kumb. 28:47-48. Nimepokea Sauti na nimeikubali
ReplyDeleteNabarikiwa sana na makala hizi
ReplyDeleteCHANZO CHA MEMA NA MAZURI YOTE
awajaze hekima yake, awape ujasiri
na afya njema viongozi wetu wote.