MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Kibaha Mjini, Nuru Magege amewaasa wanachama na viongozi Chama cha Mapinduzi (CCM) kuzisoma katiba na kanuni za chama na jumuiya zake ili kukielewa vizuri na kutenda kulingana na matakwa ya chama.
Pichani ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa matawi, serikali za mitaa na kata, yaliyofanyika ofisi za CCM Kata Pangani, Nuru alisema ni muhimu sana kwa kiongozi kufahamu kwa uhakika kanuni na katiba ili kufanya kila kitu kwa mujibu wa taratibu za chama.
“Viongozi someni katiba, someni kanuni, tuendeshe chama tukiwa tunafahamu kwa ufasaha chama kinatuagiza tufanye nini,” alisema Nuru na kuongeza kuwa tukifahamu hayo kwa ufasaha itaepusha migogoro tunapofanya maamuzi na pia tutaondoa manung'uniko katika utendaji.
Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi Nuru Magege (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Kata Pangani, Merere Mwambene.
Aidha mwenyekiti huyo wa wazazi, aliwataka wanachama na viongozi kuvaa sare kwenye kila mikutano na matukio ya chama na jumuiya zake.
“Kutakuwa na sare zenye nembo ya jumuiya ya wazazi, lakini kwa sasa mnaweza kufanya hata sare za chama,” alisema Nuru akizungumza na baadhi ya viingozi wa jumuiya waliokuweko kwenye mafunzo hayo.
Your Ad Spot
Jul 14, 2021
TUSOME KATIBA NA KANUNI, AASA NURU MAGEGE MWENYEKITI WAZAZI KIBAHA MJINI
Tags
siasa#
Share This
About Dismas Lyassa
siasa
Tags
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇