LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2021

HUYU NDIYE GILBERT KALIMA, KATIBU MKUU MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI TANZANI

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM

Kamati Kuu ya Halmashari Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi ilimteua Gilbert Kalima kuwa  Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania.


Kabla ya uteuzi huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo alikuwa Mwalimu Erasto Sima ambaye alihudumu nafasi hiyo tangu alipoteuliwa  mwaka 2018.


Kufuatia uteuzi huo bila shaka wapo wenye shauku ya kutaka kumjua vema huyu Gilbert Kalima japo si mgeni katika tasnia ya siasa.


Hadi uteuzi huo, Kalima alikuwa ni Katibu Myeka wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula.


Kalima ambaye ni Mtaalamu wa Manunuzi na Ugavi kwa ngazi ya Stashahada ya Uzamili (Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam), kama nilivyoeleza hapo mwanzo siyo mgeni katika tasnia ya Siasa.


Mwaka 1996 aliajiriwa na CCM na kufanyakazi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM kama Msaidizi wa Katibu Mkuu ambaye wakati huo alikuwa Mzee Mangula.


Kati ya mwaka 2000 hadi 2003 Kalima aliteuliwa kuwa Katibu Msaidizi (Mhasibu) wa CCM Wilaya  Kwimba na kuanzia 2003 akawa Katibu wa CCM Wilaya hiyo ya Kwimba.


Baadaye kuanzia mwaka 2006 hadi 2008 Kalima aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.


Katika hali inayoonyesha kuwa Kalima alikuwa akiendelea kuaminiwa na Chama, mwaka 2008 alitoka Kibaha Vijini na kwenda kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mkuranga.


Na kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 alikuwa Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kabla ya kuwa Katibu Myeka wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kuanzia mwaka 2016, nafasi ambayo amehitisha kuihudumu mwaka huu wa 2021 kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Wazazi Tanzania.

Gilbert Kalima Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Tanzania

1 comment:

  1. Tunashukuru kumpata katibu Mkuu Jumuiya ya wazazi Taifa. Kwa sifa alizonazo bila shaka tutaenda nae vema.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages