Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi (katikati) akizungumza muda mfupi kabla ya kuzindua Vijana Jogging kwa Tanzania nzima leo kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma leo Julai 31, 2021.
Mbio hizo za polepole maarufu kama Jogging zimeanzia kwenye viwanja hivyo na kuzunguka baadhi ya barabara za jiji la Dodoma hadi Uwanja wa Jamhuri ambapo wamefanya mazoezi laini.
Kihongosi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, amewaagiza wenyeviti na makatibu wa UVCCM wa mikoa kuanzisha Vijana Jogging katika mikoa yao na ngazi zote za chini wilayani, Kata hadi vijijini.
Amesema kuwa lengo la mpango huo wa mazoezi ni kuimarisha afya ma kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi na hasa janga la ugonjwa Uviko 19.
Amewataka watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupata chango kama alivyoonesha kwa kuchanjwa yeye siku alipozindua Ikulu Dar es Salaam.
"Msikubali vishawishi vya baadhi ya watu wasiolitakia mema Taifa letu wanaosambaza maneno yasiyofaa kuhusu chanjo.Msiwakubali, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako, nendeni mkapate chanjo mjikinge na Corona,"amesisitiza Kihongosi.
Kihongosi amemteua Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kuwa Mlezi wa Vijana Jogging Mkoa wa Dodoma. Licha Jogging hiyo kuhudhuriwa na vikundi vya Jogging vya mkoa wa Dodoma lakini pia Jogging kutoka Arusha Mjini na Iringa walishiriki.
Kihongosi akiungana vijana kufanya mazoezi laini kwenye Uwanja wa Jamhuri. |
Vijana wakiwa na bango la kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika mapambano dhidi ya CORONA.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇