RC Mtaka akihutubia kanisani hapo. Kushoto kwake ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk Dickson Chilongani.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewashauri viongozi dini na waumini wao kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Corona ambayo imezinduliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan.
RC Mtaka ametoa ushauri huo alipokuwa akihutubia katika alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Sinodi Kanisa Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika uliofanyika katika Kanisa la Anglikana Mlimwa jijini Dodoma leo Julai 31,2021.
Amesema kuwa kwa viongozi na waumini watakaojitokeza kwenda kuchanjwa ofisi yake itawaandalia utaratibu mzuri wa kupata chanjo hiyo bila matatizo.
Amewatoa hofu kuwa chanjo hiyo ni salama na ndiyo maana Rais Samia Suluhu Hassani ameizindua kwa kuanza kuchanjwa yeye, hivyo wajitokeze wenge kwenda kupata chanjo.
Amesema kuwa suala la uhai wa mtu ni mtu mwenyewe na kwamba mtu si mali ya kanisa wa serikali akifa anaondoka yeye duniani analiacha kanisa na nchi hivyo ni wajibu wa kila mtu kulinda uhai wake.
Pia RC Mtaka, amewahamasisha viongozi na waumini wao kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kupata unafuu wa matibabu mbalimbali.
Wakati akihamasisha juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko hiyo, alimwita madhabahuni Afisa Wanachama wa NHIF Mkoa wa Dodoma, Desderius Buliye ambaye alielezea taratibu za kujiunga na mifuko hiyo.
Aidha, RC Mtaka amewaelezea umuhimu wa kuijakinisha Dodoma kwa kutoa wito kwa kila kiongozi na muumini kupanda miti ya kivuli na matunda katika makazi yao.
Afisa Wanachama wa NHIF Mkoa wa Dodoma, Desderius Buliye akielezea taratibu za kujiunga na mifuko hiyo.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇