Mbunge wa Jimbo la
Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kata ya
Kiseke juu ya Bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2021/2022 na miradi
itakayotekelezwa kutokana na bajeti hiyo iliyopitishwa hivi karibuni na
Vikao vya Bunge la Bajeti
Wananchi wa kata ya
Kiseke waliojitokeza kumsikiliza Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt
Angeline Mabula wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na changamoto za
wananchi.
Mbunge wa Jimbo la
Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kata ya
Kahama juu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo
…………………………………………………………………………..
Wananchi wametakiwa
kujenga kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za ardhi na mipango miji
pindi wanapotaka kuendeleza maeneo yao hasa yale ya mijini ili
kujiepusha na hasara zinazoweza kujitokeza ikiwemo kuvunjiwa nyumba zao
kwa kutozingatia matumizi sahihi ya ardhi ya eneo husika.
Rai hiyo imetolewa na
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza
na wananchi wa kata za Kahama na Kiseke ikiwa ni muendelezo wa ziara
yake aliyoianza mwanzoni mwa wiki kwaajili ya kusikiliza kero za
wananchi, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kukumbusha
juu ya uchukuaji wa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 na kutoa
mrejesho wa vikao vya Bunge la bajeti lililoisha hivi karibuni ambapo
akawataka wananchi hao kuhakikisha kabla ya kununua eneo na kulifanyia
maendelezo kujiridhisha na matumizi sahihi ya ardhi ya eneo hilo kwa
kushirikisha ofisi za ardhi za majiji na manispaa za eneo husika,
viongozi wa maeneo yao, majirani wa pande zote ili kupunguza migogoro
isiyokuwa ya lazima na hasara kwa kuingia gharama zisizo na umuhimu
‘.. Ni marufuku
kujenga kiholela katika maeneo yote ya manispaa kwasababu
yalishatangazwa kama maeneo ya miji, Huwezi kufanya uendelezaji wowote
bila kuwa na kibali, bila kuwa na ramani, bila kuhusisha ofisi
zinazohusika ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula
akawataka wananchi kuacha kununua ardhi kiholela kwani kila kipande cha
ardhi kimepangiwa matumizi yake huku akiahidi matofali yote
yatakayohitajika katika ujenzi wa shule mpya ya msingi mtaa wa Isela
wakati wataalamu kutoka taasisi za Tanesco, Tarula na Mwauwasa wakitaja
miradi mbalimbali ya maendeleo inayoenda kutekelezwa katika maeneo hayo
Kwa upande wake
mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Masala, Afisa Tarafa
wa wilaya hiyo Ndugu Godfrey Mzava akamhakikishia ulinzi na usalama
ndani ya wilaya hiyo sambamba na kuwataka wananchi kutoa taarifa juu ya
vitendo vya kiharifu na kushiriki utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Nae mwakilishi wa
mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela, Afisa ardhi na mipango miji Ndugu
Shukran Kyando amekemea vitendo vya matumizi ya ardhi bila vibali vya
manispaa ikiwemo kuendesha biashara ya ufyatuaji wa matofali katikati ya
makazi ya watu jambo linalochangia uharibifu wa mazingira kwa kuzalisha
kelele
Moja ya wananchi
walioshiriki mkutano huo Bi Hawa Kiboto mbali na kumpongeza Mbunge Dkt
Angeline Mabula kwa ziara hiyo akaomba usimamizi zaidi wa sera ya afya
inayotaka mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano kuhudumiwa
bila gharama pindi wanapohitaji huduma ili kuokoa maisha ya mama na
mtoto pindi inapojitokeza dharula
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇