Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge akimkabidhi Ilani ya CCM Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda mjini Singida,baada ya kumuapish leo. Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge akizungumza baada ya kumuapisha mkuu huyo wa wilaya.Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Semani Mwenda akizungumza baada ya kuapishwa.Baadhi ya viongozi wa Dini Wilani Iramba wakiwa kwenye hafla hiyo ya Uapisho. .
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda akiwa na Wanafamilia yake baada ya kuapishwa
Iramba, jana
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema ishara ya utawala uliotukuka ni amani na utulivu katika maeneo ya kazi na si vinginevyo.
Dkt. Mahenge ameyasema hayo baada ya kumuapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Iramba Selemani Mwenda ambaye ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuongoza wilaya hiyo.
“Jambo la msingi ninalopenda kukuambia hakikisha kuna amani na utulivu katika wilaya yako hata ukifanya makubwa mazuri kiasi gani kama hakuna amani na utulivu mambo hayo yatafunikwa na makosa,” alisema Mahenge.
Alisema ni wajibu wa viongozi kuhakikisha ulinzi, usalama na amani vinatamalaki muda wote kuzunguka maeneo yao.
Aliongeza kwamba kazi ya kiongozi wa umma, pamoja na mambo mengine ni kuhamasisha maendeleo katika kila nyanja.
“Niwaombe sana vijana wangu wakati mnatekeleza majukumu yenu zingatieni akili za kuambiwa changanya na za kwako,” alisema Dkt. Mahenge.
Mahenge aliahidi kuwapa ushirikiano wakuu wote wa wilaya mkoani hapa lakini kwa wale watakao kuwa wachapa kazi na kuwa afadhari watofautiana kwenye misingi ya utekelezaji wa kazi watakaa na kuamua kipi wakifanye na si majungu.
Akizungumza baada ya kuapishwa Selemani Mwenda alitoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kushika nafasi hiyo na kuahidi kukidhi matarajio ya nafasi hiyo kwa kwenda kuwatumikia wananchi wa Iramba na kufuata kiapo alichoapa cha utumishi.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro wakizungumza kwa nyakati tofauti katika hafla ya kumpokea Mwenda waliahidi kumpa ushirikiano wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi wa Wilaya ya Iramba maendeleo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇