Ikulu, leo
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wanne, akiwemo Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Waziri wa zamani wa Wizara Habari, Vijana, Utamaduni na Michezi Dk. Fenella Ephraim Mukangara.
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Jaffar Haniu imesema Dk. Fenella Ephraim Mukangara ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Wengine ni Brigedia Mstaafu Aloyce Damian Mwanjile kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Khalfan Ramadhani Khalfan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Capt. Mussa Mandia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Taarifa hiyo imesema uteuzi huo unaanza leo tarehe 19 Juni, 2021.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇