LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 12, 2021

RAIS SAMIA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MUSEVENI NCHINI UGANDA, LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na kumpongeza  na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya Sherehe za Uapisho zilizofanyika katika uwanja wa Kololo Kampala nchini Uganda, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika Uwanja wa Kololo, kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni zilizofanyika katika uwanja huo uliopo Kampala nchini Uganda leo tarehe 12 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo ya Taifa la Uganda ukipigwa mara baada ya Uapisho wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni uliofanyika katika Uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni akikagua Gwaride la Jeshi la Uganda huku akiwa kwenye Gari la wazi mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Uganda katika kipindi cha muhula mwingine katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kololo, Kampala nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages