Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda (wa tatu kushoto) akifunua pazia ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Rafiki Hotel yenye hadhi ya nyota nne jijini Dodoma. Kulia ni Mmiliki wa Hoteli hiyo, Fladimiry Mallya. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu, Hokororo na Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde.
Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda akifungua rasmi Hoteli ya Rafiki ya nyota nne iliyopo karibu na Shoppers Plaza jijini Dodoma Mei 8, 2021.
WAZIRI wa Kilimo Profesa Aldof Mkenda amewaasa wawekezaji waendelee kujitokeza katika kutumia fursa ya kuwekeza katika mkoa Dodoma hasa katika ujenzi wa hoteli kubwa.
Akizungumza katika uzinduzi wa hoteli ya nyota nne ya Rafiki (Rafiki Dodoma Hotel) iliyopo eneo la Chadulu jijini hapa,Profesa Mkenda alisema maeneo ya kuwekeza katika sekta ya hoteli bado mkoani humo huku akisema fursa hiyo inapaswa kuchangamkiwa ili kukidhi mahitaji ya sasa katika mkoa huo. "
Dodoma sasa imepewa hadhi ya Makao Makuu lazima mahitaji ya nyumba kama hizi yaongezeke kutokana na watu wengi kuna Dodoma kuwa shughuli mbalimbali." Alisema Profesa Mkenda huku alisema
"Uwekezaji huu unaonyesha azma ya Serikali ya kuweka Makao Makuu Dodoma imepokewa na wafanyabiashara na hivyo kuleta fahari katika mji wa Dodoma."
Alisema siri ya mafanikio ya nchi pamoja na sekta binafsi kushiriki katika kuwekeza katika nyanja mbalimbali na kazi ya Serikali in kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi ili iweze kuchangia vyema katika pato labtaifa kupitia uwekezaji wao.
Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma Mjini Anhtony Mavunde alisema baada ya Dodoma kupandishwa hadhi ya Makao Makuu imekuwa ni jiji linaloongoza kwa ukuaji na kuwa na shughuli nyingi za kiuchumi na hivyo kusababisha mahitaji mbalimbali kuongezeka yakiwemo ya malazi. "
Hoteli hii sasa inakwenda kupunguza changamoto hiyo ,lakini pia imeongeza thamani ya eneo hili la Chadulu pia imetengeneza nafasi za ajira na wafanyabiashara wametengenezewa soko la ajira la bidhaa mbalimbali zikiwemo mbogamboga,nyama ,mayai na bidhaa nyingine nyingi ."
Alisema Mavunde Awali Mkurugenzi wa hoteli hiyo Fladimiry Mallya alisema ameamua kuwekeza Dodoma ikiwa ni sehemu ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo na zimekuwa zikitangazwa na Serikali ikiwemo ya ujenzi wa hoteli.
Ameiomba serikali iendelee kuwaunga mkono katika kutatua changamoto mbalimbali katika nyumba hizo hasa ya maji na barabara ili uwekezaji huo uweze kuleta tija kama ilivyokususdiwa na waliowekeza pamoja na Serikali ya kuongeza kipato.
Lakini pia ameiomba Serikali iweke unafuu wa kodi ya mabango ili kuonheza wigo wa wafanyabiashara kujitangaza.
Muonekano wa hoteli hiyo kwa nje.
Bwawa la kuogelea lililopo mbele ya hoteli hiyo.
Chumba chenye vitanda viwili. Kulala kwa siku moja ni sh. 100,000
Chumba cha kitanda kimoja kulala ni sh 120,000 kwa siku.
Eneo la vinywaji
Mgeni rasmi, Prof. Mkenda akiwa pamoja na mmiliki wa hoteli, Mallya, Mshauri wa masuala ya Hoteli na Utalii, Barick Daniel (kushoto) pamoja na wageni wengine waalikwa mbele ya mapokezi ya hoteli hiyo.Pro
Prof. Mkenda akifunguliwa mlango wa moja vyumba vya hoteli hiyo.
Prof. Mkenda akiangalia moja ya vyumba
Akiwasha taa sehemu ya kusomea
Waziri Mkenda akimpongeza Mallya kwa uwekezaji mzuri.
Wakiwa katika picha za pamoja na viongozi wa hoteli pamoja na wageni waalikwa.
Sasa ni wakati wa kufurahi na kunywa mvinyo
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau nakuomba uendelee kuona na kusikiliza yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa hoteli hiyo Mei ,2021......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
Very fantastic hotel I appreciate your plans,one day I will visit there. Thanks
ReplyDelete