Saa 8:33 mchana wa leo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya kusogeza mbele mechi kutoka Saa 11:00 jioni hadi Saa 1:00 usiku ikisema imepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufanya hivyo, japo haikutaja sababu.
Nusu saa baadaye Yanga SC wakatoa taarifa ya kupinga mabadiliko hayo wakisema yanakiuka kanuni inayotaka mchezo ubadilishwe muda sio chini ya Saa 24 kabla.
Yanga SC waliwasili Uwanja wa Mkapa Saa 9:30 na kufanya
mazoezi ya kuamsha misuli kabla ya kurejea vyumbani kusubiri muda wa
kuitwa na waamuzi kuingia uwanjani, lakini Saa 11:30 wakaondoka kurejea
kambini kwao.
Baadaye Simba SC nao wakaingia uwanjani kufanya mazoezi pia
kabla ya kurejea vyumbani na kisha nao kuondoka pia baada ya Saa ya Saa
1:15 usiku.
Maelfu ya mashabiki waliobaki uwanjani walianzisha vurugu kudai
warejeshewe viingilio, kabla ya Polisi kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya.
Huu ulikuwa mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana.
Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia
kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha
kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni
kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇