Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza katika mkutano na waandishi wa hbari jijini Dodoma leo, mara baada ya kupokea taarifa ya makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga Tanzania, kutoka kwa kamati maalumu iliyoundwa. Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Byabato.
Waziri Kalemani akifafanua jambo katika mkutano huo
Wanahabari wakiwa kazini
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Serikali imepokea taarifa ya ripoti ya kamati ya majadiliano ya watalaamu wa Uganda na Tanzania ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta linaloanzia Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania mara baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Katibu wa Kamati ya watalaamu wa Tanzania, ambaye pia ndiye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Masanja Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesema mradi huo utaanza mapema sambamba na kuanza kwa zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopitiwa na mradi fidia inayofikia bilioni 28.8.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia video hii, Waziri Kalemani akielezea kuhusu taarifa hiyo na umuhimu wa kuanza ujenzi wa bomba hilo pamoja na faida lukuki watakayopata watanzania ikiwemo fursa za biashara na ajira...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇