Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wanane wakiwemo Wakurugenzi wawili na Wenyeviti sita wa Taasisi mbalimbali za umma.
Taarifa tuliyoipokea jioni hii kutoka Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, imesema Rais Samia amemteua Dk. Richard J. Masika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na kwamba uteuzi huu umeanza juzi, Aprili 26, 2021, kujaza nafasi ya Marehemu Prof. Apollinary Elikana Peleka.
Pia Rais amemteua Prof. Joseph J. Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na Uteuzi huu umeanza Aprili 15, 2021. kuchukua nafasi ya Prof. Manase Peter Salema.
Wengine ni Dk. Revocatus Petro Mushumbusi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) ambaye uteuzi huu umeanza Aprili 16 2021, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ladislaus Nshubemuki ambaye amestaafu.
It
Prof. John W.A. Kondoro ambaye ameteuliwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza. Uteuzi huu umeanza Aprili 15, 2021.
Dk. Mboni A. Ruzegea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB). Uteuzi huu umeanza Aprili 16, 2021, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Ali Mcharazo ambaye amestaafu.
Prof. Esther Hellen Lugwisha kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza na uteuzi huu umeanza Aprili 15, 2021.
Kept. Ernest Mihayo Bupamba kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (Dar es Salaam Maritime Institute – DMI) baada ya kumaliza kipindi cha kwanza na uteuzi wake umeanza Aprili 15, 2021.
Prof. Makenya Maboko kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza naye uteuzi huu umeanza tarehe 15 Aprili, 2021.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇