MBUNGE wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika amesema licha ya kuwepo Muongozo wa Uwekezaji na Biashara (Blue Print), bado viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilisha mtazamo kuhusu uwekezaji.
Mwanyika aliyazungumza hayo alipokuwa akichangia utekelezaji wa Mapango wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni Dodoma, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Mchemba.
"Hiyo 'Blueprint' inaongelewa ni karatasi tu; tunatakiwa kubadilisha mtazamo kwa viongozi wa serikali katika Taasisi zinazosimamia uchumi kuanzia Benki Kuu (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na vyombo vyote vya udhibiti.
"Hawa watu wasipobadilisha mawazo na kuona sekta binafsi ni injini ya uchumi, tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu,"alisema Mwanyika.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mbunge Mwanyika akielezea kwa undani kuhusu mambo hayo na mengineyo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇