Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
MBUNGE wa Ludewa, Joseph Kamonga ameeleza wasiwasi walionao wananchi wa Ludewa kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma kama kweli utajengwa katika kipindi hiki cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano.
Mbunge Kamonga ameeleza wasiwasi huo alipokuwa anachangia bungeni Dodoma, kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano uliowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Mchemba.
Aidha Kamonga ameiomba Serikali kuwalipa kiasi cha sh. bilioni 11 wanazodai kwa muda mrefu wananchi waathirika wa miradi hiyo ambao ardhi yao imechukuliwa na hawasuruhusiwi kuiendeleza.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Mbunge Kamonga akiwapambania bungeni wananchi wa Jimbo la Ludewa....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇