Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kinywa na meno iliyokuwa ikiwalazimu wakazi wa mji wa Njombe na mkoa kwa ujumla kutafuta huduma hiyo umbali mrefu kutoka katika makazi yao na wakati mwingine kufuata mikoa ya jirani,hospitali ya Tanwat imefungua kliniki ya meno ya kisasa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kliniki hiyo ulioongozwa na Arum Mudgil mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tanwat, Bethy Liduke muuguzi mkuu wa hospitali hiyo amesema,huduma zitakazotolewa katika kliniki hiyo ni pamoja na upasuaji mdogo wa kinywa huduma iliyokuwa ikifuatwa mbali na wakazi wa Njombe.
“Kliniki hii itahudumia huduma mbali mbali kuanzia meno na matatizo yote ya kinywa lakini kuna kung’oa meno,kutibu yakipata mvunjiko lakini kubwa zaidi kuna upasuaji mdogo utafanyika hapa nipende kuwakaribisha wananchi kufika katika kliniki yetu”alisema Beth Liduke
Naye afisa utawala wa hospitali ya Tanwat Edmund Munubi amesema kliniki hiyo itakayoendeshwa na daktari bingwa imeanza kutoa huduma za kusafisha meno,kupanga,kunyoosha na kuweka meno bandia.
“Wagonjwa wa meno wanahangaika sana na huduma zilizopo kwenye mji wetu sio za kiwango kikubwa kwa hiyo tukaona haja ya kuwasaidia wengi wanao hitaji huduma”alisema Mnubi
Aidha amesema hospitali pia imeanzisha huduma maalumu kwa akina mama wajawazito kwa kutoa huduma ya gari ya kubeba wagonjwa (Ambulance) kwenye maeneo mbali mbali ya mji wa Njombe bilia ghalama yoyote wakati akina mama wajawazito wanapokuwa wamepata tatizo au kufikia wakati wa kujifungua.
“Huduma hii tunaitoa kwa akina mama wajawazito wanaoishi ndani ya Njombe mjini katika eneo linalofikika na utatupigia kwa namba zetu za dharula 0735002233 ili kuweza kusaidiwa pamoja na watoto ambao afya zao zimabadirika hasa nyakati za usiku”alisema Munubi
Kwa upande wake Antery Kiwale meneja mkuu wa misitu katika kampuni hiyo inayosimamia hospitali hiyo amesema kazi nyingi za kampuni hiyo zinafanywa na watu wenye afya njema hivyo kuendelea kuongezwa huduma katika hospitali hiyo wanaamini jamii itaendelea kuwa salama na kuongeza ufanisi na uzalishaji uchumi ndani ya jamii huku akitolea mfano binti yake aliyekuwa akipata matibabu ya Meno katika mkoa wa Dar es Salaam
“Kazi zetu nyingi zinafanyika kwa kutumia watu na bila watu wenye afya malengo yetu ya uzalishaji yatakwama,tuwapongeze sana hospitali kwa kuhakikisha watu wetu wanakuwa na afya wakati wote.tunafarijika sana hasa leo kuona kliniki hii ya Meno inafunguliwa leo ambayo itakuwa inasaidia watu waliokuwa wanakwenda mikoa mbali mbali”alisema Kiwale
Baadhi ya wananchi akiwemo Geofrey Kitwange mkazi wa Lupembe na Happy Mhiche waliofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu mbali mbali wameishukuru hospitali hiyo kwa kuongeza huduma hiyo kwa kuwa wengi walikuwa walikuwa wakifuata maeneo ya mbali.
“Wametuletea msaada mkubwa sana kwasababu wengi walikuwa wanantamani huduma iwepo karibu kutokana na changamoto ya kufuata mbali,kwa wale wasiojua natamani watambue huduma hii kwa sasa ipo karibu”alisema Happy Mhich

Arum Mudgil mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tanwat aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla ya uzinduzi wa Kliniki hiyo akishukuru uongozi wa hospitali kwa kufungua fursa ya kliniki ya meno ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo iliyokuwa ikifuatwa umabli mrefu na wakazi wa Njombe
Kushoto ni Antery Kiwale meneja mkuu wa misitu kutoka kampuni ya Tanwat na kulia ni Arum Mudgil mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tanwat wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na utoaji wa huduma ya kinywa na meno katika hospitali ya Tanwat.
Bethy Liduke muuguzi mkuu wa hospitali ya Tanwat akiwa kwenye mashine maalum ya meno wakati wa kuonyesha namna mashine hiyo inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya kinywa na Meno.
Miongomi mwa mashine iliyofungwa katika kliniki ya kinya na meno hospitali ya Tanwat ili kurahisisha huduma za kinywa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇