LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2021

MTENGA ALITAKA BUNGE LIMUENZI HAYATI MAGUFULI KWA KUWEKA BANGO LAKE ROUND ABOUT MOROGORO+video

Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga akichangia majadiliano ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zakejijini Dooma ambapo awali alishauri kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli kwa kumjengea alama ya kumbukumbu kwa kuweka bango kubwa Morogoro katika round about ya  Barabara ya Dar-Morogoro-Dodoma.

 Na Richard Mwaikenda, Dodoma
MBUNGE wa Mtwara Mjini Hassan Mtenga (CCM) ameliomba Bunge kumuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania  hayati Dkt.John Magufuli kwa kuweka picha yake katika makutano (round about) ya barabara Morogoro -Dar Es Salaam .


Akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu Mbunge huyo amesema ,hiyo itaonyesha dhahiri kwamba bunge lilikuwa linamuunga mkono.

"Hayati Rais Magufuli amekuwa ni kiongozi bora barani Afrika,na ni kiongozi ambaye marais wa Afrika walikuwa wanatamani kuiga kutoka kwake,

" Ikitupendeza pale Morogoro round about tukaweke picha yake kama ni legasambayo amaeiacha ili na sisi kama wabunge ionekne dhahiri kwamba tulikuwa tunamuunga mkono."alisema Mtenga.

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza waziri wa MajinJumaa Aweso na  Naibu Waziri wa Kilimo  Hussein Bashe kwa kuwa wasikivu wanapowasilishiwa changamoto za wananchi.

"Desemba mwaka jana nilimweleza Bashe kuhusu zao la korosho na wakala wa zao hilo TMX ,madalali hawa wanasema watanunua korosho kwa njia ya online,sasa hapa ina maana kama kulikuwa na wafanyakazi 20 maana yake watanzania hawa wote watakosa kazi na badala yake atabaki mmoja tu maana hakutakuwa na kazi za kufanya.

" Kwa hiyo naipongeza Serikali kwa kuliona hilo na kukubali TMX wakae pembeni." 

Kuhusu Aweso alisema alimfuata Waziri huyo na kumweleza mabomba yanayotumika Mtwara ni mabomba ya chama ambayo yaliwekwa na mkoloni na kwamba hata likiwekwa chujio bado yatakayotoka  pale hayatakuwa salama kwani mabomba hayo hana kitu.

Amemwomba waziri huyo kuwa na mpango wa madhubuti wa kuipatia Mtwara maji ya uhakika.

Akizungumza kuhusu ajira kwa vijana alisema Mtwara ina ardhi ya kutosh isipokuwa uwezeshwaji kwa vijana ili waitumie ardhi hiyo kwenye Kilimo ndio hakuna.

Ametumia fursa hiyo kuwekeza kwa vijana hasa katika Kilimo kwa vijana  wa Mtwara mjini ili waitumie ardhi hiyo kujiajiri lakini kubwa zaidi kujipatia kipato.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii Mbunge Mtenga  pamoja na mambo mengine akielezea jambo hilo la kumuenzi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Magufuli...



Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages