Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby akichangia Randama ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake, ameishauri serikali kurekebisha sheria ili baraza la madiwani wakiwemo wabunge waweze kuisimamia Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) kuhusu miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Aidha, Shabiby ameitaka Serikali kusitisha mkataba wa kampuni inayoweka vinasaba kwenye mafuta na kazi yake ifanywe na TBS na fedha zielekezwe Tarura kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa barabara.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video, Mbunge Shabiby akichangia juu ya masuala hayo....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇