LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 9, 2021

ASKOFU DKT CHANDE: KULIPA KODI NI AGIZO LA MUNGU, MSIHOFU KULIPA



ASKOFU Dkt Evance Chande wa Kanisa la EAGT Nazaret Ipagala, jijini Dodoma amesema kuwa watanzania wasiwe na hofu  kuogopa kulipa kodi, wanapaswa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwani  kulipa kodi ni agizo la Mungu.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kanisani kwake Aprili 8,2021 amba alinukuu Neno la Mungu kwenye Biblia linalozungumzia umuhimu wa kuitii Mamlaka iliyo madarakani na kulipa kodi.

Askofu Chande ametoa ushauri kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza wigo wa kodi na walipa kodi wapya kwa kutoa elimu  kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kwamba viongozi wa Dini wataisaidia Serikali kulihubiri hilo katika ibada zao.

Mdau, nakuoma uendelee kumsikiliza kupitia clip hii ya video Askofu Chande pamoja na mambo mengine akielezea kiundani ni jinsi gani inatakiwa kupanua wingo wa kodi....

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages