LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 18, 2021

SPIKA: TUMEPOTEZA RAIS KIPENZI ALIYEJITOA KUWATUMIKIA WATANZANIA KWA UADILIFU, BIDII NA MOYO WA KIZALENDO

Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari, leo jijini Dodoma.


CCM Blog, Dodoma

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania wamepoteza Rais kipenzi cha watu aliyekuwa amejitoa kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umahiri, bidii na moyo wa uzalendo wa hali ya Juu.


"Tumempoteza Rais wetu kipenzi aliyejitoa kuwatumikia Watanzania wote kwa uadilifu, umahiri, bidiii na moyo wa uzalendo wa hali ya juu. Kwa Niaba ya Bunge natoa pole kwa Mama Janeth Magufuli na famia ya Marehemu, Makamu wa Rais pamoja na Watanzania wote kufuatia msiba huu mzito wa Kitaifa", amesema Spika Job Ndugai alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari, leo jijini Dodoma.



Spika Ndugai amesema amepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, kilichotokea jana saa 12 jioni katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam na kutangazwa na Makamu wa Rais Samia suluhu Hassan.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages