Baadhi ya Wandishi wa Habari wakiwa kwenye mkutano Polepole akitangaza taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Hayati John Magufuli.
Baadhi ya wanahabari na watumishi wa CCM
Bendera ya CCM na Bendera ya Taifa zikipepea nusu mlingoto juu ya jengo la Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza maombolezo ya siku 21 sambamba na siku 14 zilizotangazwa na Serikali kufuatia msiba wa Mwenyekiti wa chama hicho, aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli.
Taarifa hiyo imetangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humprey Polepole katika makao makuu ya CCM, Jijini Dodoma leo akiwa na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambao ni; Katibu wa Jumuia ya Wazazi, Erasto Sima, Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT), Queen Mlozi, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Raymond Mwangwala.
Aidha, Polepole ametangazakuwa kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, kitafanyika Jumamosi Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Kwa kipindi chote cha maombolezo, bendera za CCM zitakuwa zinapepea nusu mlingoti.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video Polepole akitangaza siku hizo za maombolezo na baadhi ya viongozi na makada wa chama hicho wakielezea jinsi walivyoupokea msiba huo.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇