Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi wa waathirika wa mafuriko eneo la Nkuhungu, jijini Dodoma .
RC Mahenge akizungumza na wananchi wa eneo hilo alipokwenda kuwatembelea
Baadhi ya nyumba ambazo watu wamezihama baada ya kukumbwa na mafuriko.
Wakazi wa eneo hilo wakitega samaki kwa ajili ya kitoweo
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amewataka watu wote waliohama kwenye nyumba zao zilizoathirwa na mafuriko eneo la Nkuhungu, kutorejea tena katika nyumba hizo kwa usalama wa maisha yao hata kama maji yatakauka.
Dk. Mahenge ametoa agizo hilo alipotembelea kuona athari za mafuriko katika eneo hilo linalokadiriwa kuwa na kaya 600.
Amewataka waathirika ambao baadhi hadi sasa hawana mahali pa kuishi, kuacha kung'ang'ania kuishi eneo hilo ambalo hivi sasa ni hatarishi kwa maisha yao.
Katika hatua nyingine, Dk. Mahenge ameunda kikosi kazi kitakachofanya tathmini ya kujua nyumba zote zilizopo kwenye maji zikiwemo zilizopewa vibali vya ujenzi na wananchi waliovamia kujenga, ili serikali iangalie namna ya kuwahamishia maeneo mengine salama.
Ndugu, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia kwenye clip hii ya video ujue kwa kina yaliyozungumzwa na Dk. Mahenge, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde pamoja na waathirika wa eneo hilo....
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇