Chama Cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA) kitaadhimisha Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno kwa kutoa huduma bila malipo kwa Wananchi, watoto wenye mahitaji maalumu na Kliniki za Afya ya Uzazi, katika mikoa mbalimbali nchini kuanzia tarehe 15 - 20 Machi, 2021.
Kitaifa Maadhimisho yatafanyika Mkoani Iringa kuanzia tarehe 15 hadi 20 Machi, 2021 ambapo wananchi wa Iringa na Mikoa jirani watapatiwa Elimu, Ushauri, Uchunguzi na Matibabu ya Kinywa na Meno katika Vituo vya Afya Ngome, Ipogolo na Hospitali ya Frelimo, Huduma ya Upasuaji na Urekebishaji Midomo wazi Itatolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Tarehe 20, Machi 2021 yatafanyika Matembezi ya Uhamasishaji wa Afya ya Kinywa na Meno yatakayoongozwa na Mhe. Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuanzia Saa 12.30 asubuhi. Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima atakuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho haya.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO HAYA MWA HUU NI: “JIVUNIE KINYWA CHAKO”
(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇