………………………………………………………………………..
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson ametoa mitaji ya bure kwa Wakinamama Wajasiriamali wadogowadogo 309 ili kuwawezesha kukuza biashara zao, kila mjasiriamali amepewa jumla ya Tsh: 100,000/- ambapo tukio hilo limefanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini humo katika maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani.
Dr. Tulia amesema“Ndugu zangu nataka niwaeleze kwamba tumejipanga vizuri kuwatumikia Wananchi wa Mbeya Mjini ikiwa ni sehemu ya shukrani yatu kwenu kwa kutuamini na kutupa nafasi ya kuwatumikia. Tumejipanga vizuri kwa kuwa hii kazi tunaiweza”
“Wakati tukizungumza habari za Mwanamke, wapo watu mbalimbali bado wanayo changamoto ya namna wanavyomtazama mtoto wa kike, namna wanavyomtazama mwanamke lakini leo hii tunapozungumzia habari ya Mwanamke Mbeya Mjini tumechagua Mwanamke katika kutuwakilisha kwenye nafasi ya Ubunge”- Dr. Tulia Ackson
“Siku ya leo tumekusanyika hapa kwa ajili ya kuzungumza yanayotusibu Wakinamama, Wakinamama tunayo changamoto inayotusibu ikiwemo suala la uwezeshaji kiuchumi na hata tunapotaka kukopa tunahitajika kuwa na dhamana ambazo wakati mwingine hatuna. Siku ya leo tutawawezesha Wakinamama 309 ambao ni wachache kati ya wengi baada ya kufanya michujo”- Dr. Tulia Ackson
“Wakinamama hawa ni Wajasiriamali wadogowadogo ambao wengi wao mitaji yao ni chini ya Tsh: 50,000/- na sisi leo tutawapatika kila mmoja mtaji wa jumla ya Tsh: 100,000/- ili kuongeza chachu ya biashara yake ambayo anaifanya huko na huu utaratibu utakuwa mwendelezo kila mwaka na huenda mwakani ikawa mikubwa zaidi na hata kuwafikia watu wengi zaidi ya hawa”-Dr. Tulia Ackson
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇