LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 6, 2021

WATUMISHI WANAWAKE EWURA WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO NJITI KITUO CHA AFYA MAKOLE DODOMA


Mwenyekiti wa wanawake TUGHE tawi la EWURA Bi Herieth Kasilima,akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba kwa watoto Njiti katika Kituo cha Afya Makole leo March 6,2021 jijini Dodoma.

Kaimu Mganga mfawidhi kituo cha Afya Makole Dkt Tumain Kapungu akiwashukuru  watumishi wanawake kutoka EWURA kwa kuwakabidhi  msaada wa vifaa tiba kwa Watoto Njiti  vyenye thamani ya milioni tano leo March 6,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wanawake kutoka EWURA wakiwajulia hali wakina mama wenye watoto Njiti (hawapo pichani) mara baada ya kuwatembelea na kuwapa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni tano leo March 6,2021 jijini Dodoma.

 Mwenyekiti wa wanawake TUGHUE Tawi la EWURA Bi Herieth Kasilima,akimkabidhi Mfano wa Hundi ya shilingi milioni tano Matron wa Kituo cha Afya Makole Glays Tumbo mara baada ya kutembelea Kituo hicho na kutoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto Njiti  leo March 6,2021 jijini Dodoma.

  

Watumishi wa EWURA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Makole mara baada ya kutembelea na kukabidhi msaada wa vifaa tiba kwa watoto Njiti katika Kituo hicho vyenye thamani ya shilingi milioni tano leo March 6,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka watumishi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji hapa nchini EWURA wamekabidhi msaada wa vifaa tiba kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Watoto njiti) vyenye thamani ya milioni tano (5,000,000)katika kituo cha afya Makole kilichopo Jijini Dodoma.

Akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kwa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Mwenyekiti wa wanawake TUGHE tawi la EWURA Bi. Herieth Kasilima, amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake wameona watoe msaada huo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ili waweze kuhudumiwa.

“Niishukuru Bodi,Menejimenti ya EWURA kwa kutuwezesha leo kutoa misaada hii naamini itakuwa faraja kwa wazazi wanaopata watoto njiti kupitia msaada huu watahudumiwa na tunaamini fedha hii itawezesha kununua vifaa vinavyohitajika” ameeleza Bi Herieth.

Bi.Herieth emesema baada ya EWURA kupata taarifa kuwa kituo hicho kipo katika mpango wa kuanzisha huduma hiyo, wameamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuweza kukamilisha kwa wakati wodi maalumu kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika kituo hicho.

Ameishukuru bodi ya wakurugenzi EWURA kwa kuidhinisha wanawake hao wakatoe msaada  huo kwa kuwa wanaamini vifaa vikinunuliwa vitaweza kusaidia jamii ya wengi hasa wanaozaliwa katika kituo hicho hata katika maeneo mengine watakaopelekwa katika kituo hicho.

Akipokea msaada huo Kaimu Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Makole Dkt Tumaini Kapungu amewashukuru watumishi wanawake kutoka EWURA kwa kuona haja ya kutoa msaada huo kwa sababu hospitali imekuwa ikipata watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na wao wameanza kukarabati wodi kwa ajili ya watoto hao.
Bi.Kapungu ameeleza kuwa msaada huo utachangia sehemu kubwa katika kununua vifaa kwa ajili ya wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati inayotarajiwa kuanza kutoa huduma hiyo hivi karibuni

Mganga Mfawidhi huyo amewaomba watumishi wa mashirika na taasisi nyingine kuona namna ya kusaidia kwa kutoa misaada kama hiyo kwa sababu uhitaji bado upo kwa kuwa vifaa vinavyohitajika katika wodi hiyo vinathamani ya shilingi milioni ishirini na saba (27,000,000) ikiwa ni pamoja na ukarabati wa wodi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages