Baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Simba SC ya Tanzania, Klabu ya El Merreikh ya Sudan imethibitisha kumfuta kazi Kocha Mkuu wa Kikosi hicho, Nasreddin Nabi pamoja na Benchi lote la Ufundi, Merreikh imemfuta kazi Kocha huyo kutokana na matokeo mabaya yaliyopatikana hivi karibuni.
Chanzo cha Mtandao (Mwanaspoti) kimeripoti kuwa Kocha Nabi amefutwa kazi na Uongozi wa miamba hiyo ya Soka kutoka Sudan ikiwa ni baada ya kuifundisha ndani ya siku 34 tu akipokea mikoba kutoka kwa Kocha Mserbia Midrag Jesic Februari 2 mwaka huu.
Matokeo ya 0-0 dhidi ya Simba SC yameiweka pabaya, El Merreikh kufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi ambapo hadi sasa wanaburuza mkia wakiwa na alama 1 pekee huku wakifungwa michezo miwili kati ya mitatu waliocheza kwenye Kundi A la Michuano hiyo.
Mchezo wake wa kwanza wa Michuano hiyo, El Merreikh walipoteza kwa kichapo cha bao 3-0 ugenini dhidi ya Al Ahly SC ya Misri, walifungwa bao 1-4 nyumbani na AS Vita Club ya DR Congo kabla ya sare ya 0-0 nyumbani dhidi ya Simba SC ya Tanzania.
March 16, 2021 El Merreikh watalazimika kusafiri hadi Dar es Salaam, Tanzania kuwafuata Simba SC katika mchezo wa raundi ya nne ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi ikiwa ni mchezo wa Kundi A.
Simba SC baada ya sare ya 0-0 dhidi ya El Merreikh wataendelea kuongoza Kundi A la Michuano hiyo wakiwa na alama Saba wakisubiri mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya AS Vita Club kukamilisha mzunguko wa nne wa Kundi hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇