Na Richard Mwaikenda, Dodoma
ASKOFU wa Kanisa la EAGT Nazaret, Dk. Evance Chande amepiga marufuku waumini kuingia kanisani,ofisini kwake bila kunawa mikono ikiwa ni tahadhari dhidi ya janga la corona.
Akihubiri hivi karibuni katika kanisa lake lililopo Ipagala, jijini Dodoma, Askofu Dk. Chande amewatahadharisha waumini wake kuwa pamoja na kumtegemea Mungu katika mapambano dhidi ya janga la corona, wasiache mlango wazi kwa kusahau tahadhari zingine ikiwemo kunawa mikono na kuvaa barakoa walizozishona wenyewe.
Amesema kwa kujali hilo ndiyo maana katika milango ya kuingilia kanisani na ofisini kwake ameweka maji na sabuni ili kabla ya waumini kuingia wanawe mikono.
"Unapomtegemea Mungu, usiache mlango wazi. pale nje tumeweka ndoo za maji ya kunawa, mlangoni usiingie ndani bila kunawa, takasa mikono na ukisha ingia kaa 'social distance' na uhakikishe unavaa barakoa na barakoa nzuri ni ile uliyoishona mwenyewe,"amesisitiza Dk. Chande huku akishangiliwa na waumini.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Dk. Chande akiwapiga msasa waumini kuhusu mapambano dhidi ya janga la corona...
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇